Lionel Messi afunga na kutwaa kombe akiwa na Inter Miami

 

Lionel Messi amepongezwa kama mchezaji bora duniani wakati akifunga goli lake la 10 katika michezo saba na kuisaidia Inter Miami kutwaa kombe la kwanza.

Raia huyo wa Argentinian alifunga goli kwenye kona ya juu ya goli kwa shuti la nje ya boksi na kuipatia Miami goli la kuongoza dhidi ya Nashville SC katika fainali ya kombe la ligi.

Fafa Picault alisawazisha goli hilo na mchezo ukaenda kwenye mikwaju ya penati, ambapo Inter Miami iliipuka na ushindi wa magoli 10-9.

Chapisha Maoni

0 Maoni