Bei ya ngano yapanda ghafla katika soko la dunia

 

Bei ya ngano imepanda ghafla katika soko la dunia, baada ya Urusi kusema itachukulia meli zinzoenda kwenye bandari ya Ukraine kama maeneo inayoweza kuyashambulia.

Wiki hii Urusi imejitoa kwenye makubaliano ya kuruhusu usafiri salama kwa meli zinazobeba ngano kutoka Ukraine kupitia Bahari Nyeusi.

Msemaji wa Ikulu ya Marekani ameituhumu Urusi kwa kupanga kuilaumu Ukraine kwa kushambulia meli za kiraia.

Bei ya ngano kwenye soko la Ulaya imepanda kwa asilimia 8.2 jana, kutoka siku iliyopita na kuwa €253.75 (£220; $284) kwa tani moja, wakati mahindi yamepanda kwa asilimia 5.4.

Ngano Marekani bei yake imepanda kwa asilimia 8.5, ikiwa ni kiwango cha juu kabisa tangu Urusi iivamie Ukraine Februari 2022.


Chapisha Maoni

0 Maoni