Polisi watanda kudhibiti maandamano kila kona Kenya

 

Ulinzi umeimarishwa nchini Kenya kuelekea siku ya pili ya maandamano yaliyopangwa kufanyika kwa siku tatu yaliyoitishwa na chama cha Azimio.

Maandamano hayo yaliyoanza jana yameshuhudia kuwapo kwa ulinzi mkali wa polisi waliowekwa kwenye maeneo hatarishi kwa usalama nchini humo.

Wilaya ya Kati ya Kibiashara imezingirwa na makundi ya polisi waliowekwa kuwadhibiti waandamanaji wasiingie kati kati ya Jiji la Nairobi.

Wapinzani wameitisha maandamano hayo kushinikiza kupunguzwa kwa gharama za maisha na kubadilishwa kwa Sheria ya Fedha ya 2023.

Chapisha Maoni

0 Maoni