Ukatili waliofanyiwa watoto waliouawa Shakahola hausimuliki

 


Watoto ndio waliokuwa wa kwanza kulengwa kufunga hadi kufa katika kutekeleza mahubiri ya siku za mwisho katika dhehebu la kanisa tata lililopo Shakahola nchini Kenya, taarifa mpya zimeeleza.

Maelezo hayo mapya yametolewa wakati polisi wakiendelea na uchunguzi na zoezi la ufukuaji wa makaburi ya watu wengi ambapo hadi sasa miili 200 imepatikana.

Aliyekuwa msaidizi wa muhubiri ameiambia New York Times kwamba watoto waliuawa kwanza kwa kuamriwa kufunga wakiwa juani ili wafe haraka.

Msaidizi huyo Titus Katana amesema kwamba waliofuatiwa kuagizwa kufunga hadi kufa ili wakutane na muokozi wao Yesu Kristo walikuwa ni wanawake.

Katana ambaye anaisaidia polisi, ameeleza ukatili waliofanyiwa watoto ukiwemo wa kufungiwa kwenye vipanda kwa siku tano bila chakula wala maji.

Mchungaji Mkuu wa Kanisa hilo Paul Mackenzie mbali na kuwaagiza waumini wake wafunge hadi kufa alikuwa akiwahubiria wasiende shule wala wasiende hospitali.


Baadhi ya makaburi yaliyokwisha fukuliwa eneo la Shakahola na miili ya watu kutolewa na kuhifadhiwa kwa ajili ya uchunguzi zaidi.

Chapisha Maoni

0 Maoni