Barcelona watwaa ubingwa wa La Liga mapema

 


Barcelona wametwaa ubingwa wa ligi ya La Liga tangu 2018-18, huku wakiwa na michezo minne mkononi baada ya kupata ushindi wa aina yake dhidi ya Espanyol.

Barcelona walikua wanaongoza kwa mabao 3-0 hadi mapumziko, Robert Lewandowski akifunga goli lake la 20 la msimu huu kabla Alejandro Balde kuongeza la pili.

Lewandowski aliongeza goli la tatu kwa Barcelona kabla ya mpira wa kichwa uliopigwa na Jules Kounde kufanya matokeo kuwa nne 4-0.

Espanyol walipata magoli yao ya kufutia machozi kupitia kwa Javier Puado na Joselu lakini bado wanabakia wakihaha kujinusuru kutoka mkiani.

Barcelona wanaongoza kwa pointi 85, wakiwa na tofuati pointi 14 na wapinzani wao Real Madrid, waliona alama 12 za kutafuta katika michezo iliyobakia.

Chapisha Maoni

0 Maoni