Samia Complex kujengwa Ikulu Chamwino

 

Rais Samia Suluhu Hassan amesema bado kuna kazi nyingi za kufanya katika eneo la Ikulu mpya ya Chamwino ikiwemo ujenzi wa Samia Complex.


Akizungumza katika uzinduzi wa Ikulu hiyo May 20 Rais Samia amesema hatua inayofuata ni ujenzi wa jengo la kisasa ambalo limepewa jina Samia Complex ambapo kutakuwa na ukumbi wa mikutano wa watu 3,000, nyumba za viongozi haswa majirani wa EAC na SADC.



Katika eneo hilo pia kutakuwa na Zanzibar Lounge, EastAfrica Lounge, uwanja wa golf, njia ya ndege, viwanja vya michezo mbalimbali , sehemu za historia za viongozi wa nchi.


Rais Samia amesema michoro ipo tayari serikali inatafuta fedha kwaajili ya kuanza ujenzi huo.

Chapisha Maoni

2 Maoni

Bila jina alisema…
Ameanza kujipakulia manyama
Bila jina alisema…
Kazi iendeleeeee