Nani wa kuvunja ubabe wa mabingwa wa EPL Manchester City ?

 

Manchester City ambayo imetwaa kwa mara ya tano kombe la EPL katika miaka sita inaacha maswali ya nani haswa ataweza kuizuia timu hiyo kulitwaa kombe hilo tena katika ligi hiyo na kuzima utawala wa kocha Pep Guardiola.

Manchester City, ambayo imetwaa ubingwa huo jana baada ya Arsenal ambayo ilionekana mwaka huu huenda ingetwaa kombe hilo, kukubali kichapo kutoka kwa Nottingham Forest jana Jumamosi na kuzima ndoto yao.

Hakika Manchester City imedhamiria kutawala Ligi Kuu ya Uingereza na kuzikata maini timu za ligi hiyo zinazojiimarisha kutwaa kombe hilo, ambapo kila mwaka City imeonekana kujiimarisha zaidi na kulizoea kombe hilo.

Manchester City, pia imekuwa timu ya kwanza ya Ligi Kuu ya Uingereza kushinda kombe la ligi hiyo kwa misimu mitatu mfululizo, tangu majirani zao Manchester United kufanya hiyo katika misimu ya 2006-07, 2007-08 and 2008-09.

Kocha Pep Guardiola amelitwaa mara tano kombe la ligi kuu ya Uingereza tangu ajiunge na Manchester City mwaka 2016

Chapisha Maoni

0 Maoni