Mashabiki 12 wafa uwanjani El Salvador

Watu wapatao 12 wamekufa baada ya kundi kubwa la mashabiki kusukumana getini baada ya geti la uwanja wa soka kufungwa Jijini San Salvador nchini El Salvador.

Tukio hilo limetokea katika mchezo baina ya timu za Alianza na Santa Ana-based katika dimba la Fas at Cuscatlán. Mchezo huo ulisitishwa mara moja.

Rais wa El Salvador Nayib Bukele amesema kwamba tukio hilo halikubaliki na kusema uchunguzi wa kina utafanywa.

Chapisha Maoni

0 Maoni