Marekani imesema kwamba itawaruhusu washirika wake wa
Magharibi kuipatia Ukraine ndege za kisasa za vita, zikiwamo zinazotengenezwa
Marekani za F-16 ili kuisaidia uwezo wa kivita.
Mashauri wa Usalama wa Taifa wa Marekani Jake Sullivan,
amsema Rais Joe Biden amewaeleza washirika wenzake wa G7 kuhusiana na uamuzi
huo Ijumaa.
Vikosi vya Marekani pia vitawafundisha marubani wa Ukraine jinsi
ya kutumia ndege zake, Bw. Sullivan amesema.
Ukraine iemekuwa ikiomba kupatiwa ndege za kivita zenye
uwezo zaidi, Rais Volodymyr Zelensky amepongeza uamuzi huo na kusema kuwa ni wa
kihistoria.
Kisheria, nchi zinaruhusiwa kuuza ama kusafirisha vifaa vya
kivita vinavyotengenezwa na Marekani iwapo tu Marekani itaruhusu, hivyo rukhsa sasa
ndege za F-16 kupelekwa Ukraine inayopigana na Urusi.
Hata hivyo, hadi sasa hakuna serikali yoyote iliyothibitisha
kwamba itaipatia Ukraine ndege hizo za kisasa.
0 Maoni