Jimmy Butler aibeba Miami Heat

 

Mchezaji Jimmy Butler ameifungia Miami Heat pointi 27 wakati wakiibwaga Boston Celtics kwa alama 111-105 na kuongoza ushindi wa 2-0 katika mfululizo wa fainali za Eastern Conference

 

Butler alifunga pointi nane katika robo ya mwisho, huku wakiwa nyuma kwa pointi 96-89, na kuparurana na Grant Williams wa Boston.

Katika mchezo huo Butler alipata rebounds sita, alisaidia kupokonya mipira mara tatu, wakati Martin akifunga pointi 25.

Chapisha Maoni

0 Maoni