Maajabu ya Ikulu ya Chamwino Dodoma


 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Samia Suluhu Hassan leo amezindua Ikulu mpya ya Chamwino Mkoani Dodoma.


Eneo la Ikulu ya Dodoma ni zaidi ya mara 200 ya eneo la Ikulu ya Dar es Salaam ikiwa na ukubwa wa eneo la ekari 8,473.



Ukubwa huo unaelezwa kuwa  ni zaidi ya mara 15 ya ukubwa wa Hifadhi ya Taifa ya Saanane, Mwanza.

Katika eneo hilo lenye mandhari ya kuvutia kutakuwa pia na wanyamapori na hivyo kutoa uwezekano wa Ikulu kuwa kivutio cha utalii.

Ikulu la Dar es Salaam ina ukubwa wa eneo la ekari  41 na ya Dodoma ni ekari 8,473.

Rais Samia Suluhu Hassan amesema Ikulu hii ni kilele katika azma ya Serikali kuhamia Dodoma. Safari ya miaka 50 kufikia siku hii ni ya demokrasia kwani nia ya kuhamia Dodoma ilipitishwa na Halmashauri Kuu ya TANU mwaka 1973, baada ya kura ya maoni katika matawi yake nchi nzima. Safari hii ina mchango wa namna yake kwa kila awamu iliyowahi kuiongoza nchi yetu: 



1. Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere


2. Alhaji Ali Hassan Mwinyi


3. Hayati Benjamin William Mkapa


4. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete


5. Hayati Dkt. John Pombe Magufuli


Uzinduzi rasmi wa Ikulu yetu ni tukio kubwa la historia kwa Taifa letu. Tuungane sote kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutuwezesha kufikia hatua hii adimu na adhimu, miaka 50 toka Serikali ilipoweka azimio la kuhamisha Makao Makuu ya Nchi kutoka Dar es Salaam kuja Dodoma.


Chapisha Maoni

0 Maoni