Hayati Magufuli ameandika hadithi yake


Rais Samia Suluhu Hassan amesema hayati John Pombe Magufuli ameandika historia kwa kutekeleza kwa vitendo maono ya  ujenzi wa Ikulu ya kisasa Dodoma.

Rais Samia ameyasema hayo baada ya uzinduzi wa Ikulu ya Chamwino Dodoma na kusema Katika utekelezaji wa wazo hilo la kuhamishia makao makuu ya Serikali jijini humo  hayati Magufuli hawezi kusahaulika. “ ameandika hadithi yake. Hatutoweza kuandika historia ya shughuli hii bila ya kuwepo kwa tahariri ya mchango wake mkubwa.” amesema 



Rais Samia alichukua hatamu baada ya kifo  cha hayati John Magufuli Machi 2020 na kuahidi kuendeleza  mema yaliyopo,na  mema mapya kwa misingi ya kaulimbiu ya Kazi Iendelee.


Amesema hii ni historia kwani ni Kwa mara ya kwanza Watanzania kuweza  kujenga Ikulu  kwa kutumia rasilimali zao na kutumia wataalamu wetu wa Kitanzania tofauti na ujenzi wa Ikulu yetu ya Dar es Salaam.


Aidha ametambua mchango wa askari Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) walioshiriki kikamilifu katika ujenzi wa Ikulu hiyo “Eneo hii lilikuwa ni mwitu, limejaa wanyama wakali kama nyoka ila vijana wa SUMA JKT wamefanya kazi kubwa sana, kwa uzalendo na wameacha alama kubwa kwa taifa hili" amesema 



Vijana (JKT)wamefanya kazi kubwa sana kwa uzalendo, eneo hili lilikuwa limejaa wanyama wakali, limejaa manyoka lakini vijana hawa wamefanya kazi bila kuogopa bila kuchoka.


Hakusita kurusha jiwe kwa waliobeza safari ya Dodoma na kusema “Kwa wale waliokuwa na mashaka ya kutimia kwa shughuli ya kuhamia Dodoma, kwa sasa wameshaamini kwamba hakuna kurudi nyuma. 

Tupo Dodoma, Dar es Salaam tutakwenda kupokea wageni wetu wa kitaifa, tutakwenda kufanya kazi zinazopaswa kufanywa Dar es Salaam.” Rais amesema Samia 


Chapisha Maoni

0 Maoni