Rais Samia atoa neno miaka 98 ya Alhaji Ali Hassan Mwinyi


Rais Samia Suluhu Hassan amemtakia heri ya kutimiza miaka 98 Rais wa awamu ya pili Alhaj Ali Hassan Mwinyi ikiwa ni pamoja na kumshukuru kwa utumishi na busara zake kwa nchi.


Rais Samia kupitia akaunti yake katika mtandao wa twita ameandika “Nakutakia kheri mzee wetu na Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Alhaji Ali Hassan Mwinyi unapotimiza umri wa miaka 98.


Tunaendelea kukushukuru kwa utumishi wako kwa nchi yetu na busara zako. Nakuombea Mwenyezi Mungu aendelee kukukirimia neema zake, akujalie furaha na siha njema.”



Kwa upande wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Hussein Mwinyi ambaye ni mtoto wa Alhaj Mwinyi ameandika kupitia mtandao wa twita akimtakia  heri na kuandika yafuatayo



“Nakutakia kheri mzee wetu na Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Alhaji Ali Hassan Mwinyi unapotimiza umri wa miaka 98. Tunaendelea kukushukuru kwa utumishi wako kwa nchi yetu na busara zako. Nakuombea Mwenyezi Mungu aendelee kukukirimia neema zake, akujalie furaha na siha njema.”


Historia 

Mheshimiwa Alhaj Ali Hassan Mwinyi alizaliwa Kivule, Mkuranga,  mkoa wa Pwani  tarehe 5 mei, 1925. 


Mstaafu  Alhaj  Ali Hassan Mwinyi aliongoza  Serekali ya Awamu ya Pili aliingia madarakani rasmi tarehe 5 Novemba 1985.


Kabla ya hapo mwaka 1984 alichaguliwa kuwa Rais wa Zanzibar na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 


Kuhusu elimu Alhaj Mwinyi ana cheti cha umahiri wa lugha ya Kiingereza, alichohitimu katika taasisi ya Regent, Uingereza mwaka 1960 na cheti cha umahiri wa lugha ya Kiarabu alichohitimu, Cairo, Misri, mwaka 1972-74. 


Kwa upande wa kazi  alikuwa mwalimu wa shule za msingi za Mangapwani na Bumbwini, Zanzibar,  na baadae  alijiunga na chama cha Afro Shiraz(ASP) mwaka 1964 na kushika nyadhifa mbali mbali za serekali ya Zanzibar na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kama vile katibu mkuu, Wizara ya Elimu Zanzibar 1963, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwaka 1970 na kati ya mwaka 1982 hadi 1983 alikuwa Waziri wa Afya, Wizara ya Mambo ya Ndani, Maliasili na Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Misri.

 

Chapisha Maoni

2 Maoni

Bila jina alisema…
Hongera mzee umekula chumvi ya kutosha kula chuma hichooo
Bila jina alisema…
Mzee mwenye sifa ya kuwa rais katika nchi mbili tofauti