Bajeti ya kilimo yapaa kwa asilimia 29

 

Waziri wa Kilimo Hussein Bashe ameliomba Bunge kuidhinisha jumla ya shilingi bilioni 970,785,619 katika mwaka wa fedha 2023/24 ikiwa ni ongezeko la asilimia 29 ya bajeti ya mwaka 2022/23.



Waziri  Bashe ameyasema hayo leo   Mei 8, 2023 wakati akiomba kuidhinishiwa fedha hizo na Bunge ambapo kati ya fedha hizo, Shilingi 767.83 bilioni ni fedha za maendeleo.


Kwa mujibu wa Bashe  mwaka 2022/2023 fedha zilizoidhinishwa zilikuwa ni shilingi 751.12  bilioni ambapo fedha za maendeleo zilikuwa shilingi 569.97 bilioni.

Chapisha Maoni

0 Maoni