Wine yaokoa maisha ya mwanamke

 


Mwanamke nchini Australia mwenye umri wa miaka 48 ameweza kuishi siku tano akiwa amekwama msituni kwa kula pipi na kunywa wine chupa moja.

Mwanamke huo Lillian Ip alikuwa kwenye safari fupi aliyoianza siku ya Jumapili, akisafiri kwenye barabara inayokatiza kwenye msitu mzito katika jimbo la Victoria.

Lakini kwa bahati mbaya mwanamke huyo akakatiza barabara yenye kikomo, na gari lake kukwama kwenye matope.

Mwanamke huyo ambaye si mnywaji wa kileo, alikuwa na chupa ya wine tu kwenye gari ambayo alikuwa ameinunua kwa ajili ya kuitoa kama zawadi.

Baada ya kukwama kwa siku tano, mwanamke huyo alibainika na kikosi cha dharura Ijumaa baada ya kumuona wakitumia helkopta.

Chapisha Maoni

0 Maoni