Miili ya watu yafungwa na mablanketi DRC, 400 wafa hadi sasa

 

Watu zaidi ya 400 wamekufa kufuatia mafuriko na maporomoko ya ardhi yaliyovikumba vijiji viwili mashariki mwa Jamhuri ya Demokrasia ya Congo (DRC) wiki iliyopita.

Mamlaka za nchi hizo awali zilisema watu 200 wamekufa kufuatia mvua kubwa ya masika iliyonyesha Alhamisi.

Katika baadhi ya vijiji karibu na fukwe za ziwa Kivu, watu wamekuwa wakifukua matope kwa kutumia mikono yao wakihaha kuwasaka ndugu zao waliopotea.

Watumishi wa kujitolea wa Shirika la Msalaba Mwekundu la DRC hawana mifuko maalum ya kuhifadhia maiti.

Miili ya watu waliokufa imerundikana ikiwa imefungwa kwenye mablanketi katika vijiji vya Bushushu na Nyamukubi Kusini mwa Mkoa wa Kivu.

Chapisha Maoni

0 Maoni