Rais Samia atoa mwezi mmoja vibali ujenzi wa minara kutolewa


Rais wa Tanzania Dk Samia Suluhu Hassan ameagiza vibali vya minara  iliyosainiwa leo visizidi zaidi ya mwezi mmoja  viwe vimetoka.


Rais Samia amesema hayo katika hafla ya utiaji  saini Mikataba ya miradi ya kufikisha huduma za mawasiliano ya Simu katika kata 763 nchini ambapo amewaonya viongozi wanaochelewesha.

“Wale wenye makoti mazito ambayo hayainui mikono wakati wa kusaini naomba makoti yavuliwe ili yawekwe kwenye kiti ili watoe vibali kisheria kwa kufuata kanuni tulizojiwekea” amesema Rais Samia 



Amesema kumekuwepo na urasimu katika utoaji wa vibali “nlikuwa nazungumza na wizara wakaniambia ili mnara usimame  unachukua hata miezi sita kupata kibali kutoka kwa taasisi husika sasa tutaitana na wale wote wanaohusika na mambo ya utoaji wa vibali”


Chapisha Maoni

0 Maoni