Yanga bingwa ligi kuu 2022/23


Yanga Sc wametwaa ubingwa wa Ligi kuu bara kwa msimu wa 2022/23 baada ya kufikisha alama 74 ambazo haziwezi kufikiwa na timu yoyote kwenye NBCPL msimu huu.
Yanga SC imetwaa ubingwa wa Ligi kuu kwa mara ya pili mfululizo ikiwa ni kombe la 29 kihistoria, wakiwa wamesalia na mechi mbili mkononi.


Mechi ya ushindi imepigwa katika Chamanzi Azam Complex kwa kuwanyuka bila huruma Dodoma Jiji goli 4 kwa 2.


Goli za Yanga zimetiwa kimiani na Musonda 37 Mudathir Yahya kunako dk ya 70' na 90+4

na Farid Musa dk 87 , Goli za Dodoma jiji zimetiwa kambani na Opare dk 58 na Seif dk 67

Chapisha Maoni

1 Maoni

Bila jina alisema…
Bingwa ni bingwa tu