Rais William Ruto uso kwa uso na Raila Odinga

 


Rais William Ruto na mpinzani wake mkuu Raila Odinga wamepeana mikono kwa mara ya kwanza tangu kumalizika kwa uchaguzi mkuu Agosti nwaka 2022.

Raila ambaye waziri mkuu mstaafu amekutana na Rais Ruto muda huu ambapo wawili hao wanahudhurika kwenye maziko ya shujaa wa vita ya Mau Mau Mukami Kamathi.

Kitendo hicho cha wanasiasa hao kusalimiana hadharani kwa mara ya kwanza kilimevutia waombolezaji wanaohudhuria maziko hao.

Katika maziko hayo Raila alisalimiana pia na Naibu Rais wa Kenya Rigathi Gachagua pamoja na Waziri Musalia Mudavadi.

Akiongea kwenye maziko hayo Mbunge wa Naivasha Jayne Kihara alimuomba Raila Odinga kuacha maandamano ili serikali ifanyekazi.

"Raila nakuomba uwache serikali ifanye kazi, usirudi kwa barabara," alisema mbunge huyo.

Chapisha Maoni

0 Maoni