Rais Samia akiri pengo la Membe halizibiki

Rais  Samia Suluhu Hassan amekiri kuwa pengo aliloacha aliyekuwa Waziri wa Mambo ya nje na mwanadiplosia Benard Membe haliwezi kuzibika.

Rais Samia ameyasema hayo leo wakati akitoa salamu za rambirambi katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam kwenye hafla ya kuaga mwili wa marehemu Membe.


Amesema Kifo cha Membe kimewashtusha wengi ndani na nje ya nchi kwani alikua mashuhur, msiba huu si familia pekee na kuahidi  serikali ipo  pamoja kwa hakika nguzo kuu imepotea.



Amesema, katika vitu mwanadamu hawezi kuzuia ni siku ya kufa na siku ya kuzaliwa.


“Hata kama Dk atapanga operesheni siku ya kuja kwako, kama Mungu hajapanga uzaliwe basi kitatokea chochote tu na operesheni haitafanyika.” Amesema Rais Samia 


Amesema, binafsi alikua na Membe kwenye nyakati tofauti katika medali za siasa, alikua mchapakazi, kifo chake kimeacha pengo si tu kwa taifa lake hata kwa mataifa aliyoyatumikia.


Chapisha Maoni

0 Maoni