Rais Samia afanya uteuzi mpya


 Rais Samia Suluhu Hassan amemteua Mkurugenzi Mtendaji Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania  (TPDC), Mussa  Makame kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri na Uwekezaji wa Mfuko wa Mafuta  na Gesi.

Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu Zuhura Yunus  imesema Rais Samia  pia amewateua wajumbe wanne wa bodi hiyo akiwemo Dkt. Suleiman Missango, Meneja Msaidizi Kurugenzi ya Utafiti na Sera, Benki Kuu ya Tanzania (BOT).

Afisa Fedha Mwandamizi kutoka Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Safiel Msovu.


Mwingine ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Express Microfinance company Ltd, Shogholo Msangi na aliyekuwa  Mhasibu Mkuu wa Serikali, Mwanaidi Athuman Mtanda.


Uteuzi huo umeanza Mei 11, mwaka huu.

Chapisha Maoni

0 Maoni