Membe kuzikwa jumanne Lindi


 Mwili wa aliyekuwa Waziri wa mambo ya nje Benard Membe utaagwa Jumapili, May 14, 2023, katika viwanja vya Karimjee, kisha utasafirishwa kwenda kijijini kwao, Chiponda Mkoani Lindi na maziko yatafanyika siku ya Jumanne, May 16, 2023.


Msemaji wa Familia ya Bernard Membe, Mustafa Kambona, ametangaza ratiba hiyo mazishi ya Membe.




Awali akizungumza na waandishi wa habari daktari wa Membe aliyefahamika kwa jina Prof.Harun Nyagori  amesema Membe hakuwahi kuwa na ugonjwa wowote wa magonjwa sugu kama kisukari, magonjwa ya moyo,  presha hakuwahi kuwa nayo.


Prof Nyagori amesema marehemu May 11  alipata homa ndogo ya kifua, akipata shida ya kukohoa na kubanwa kifua na ilipofika usiku wa kuamkia alfajiri ya leo alishindwa kupumua ghafla akakimbizwa Hospitali.


“Kwa kifupi maradhi haya yanatokana na virusi ambavyo vinazunguka vinaingia kwa njia ya hewa vinasababisha mgando kwenye mfumo wa mapafu, damu inakuwa nzito hiyo ndio imesababisha kifo cha Mh.Membe”

Chapisha Maoni

0 Maoni