Wakili Sungusia arithi mikoba ya Prof Hoseah TLS

 

Wakili Harold Sungusia amechaguliwa kuchaguliwa kuwa Raisi wa Tanganyika Law Society (TLS) akirithi mikoba ya Prof Edward Hoseah ambaye amemaliza muda wake.


Sungusia ametangazwa mshindi kwa  mwaka 2023-2024 kwa kupata kura 748 kati ya kura 825  huku Aisha Sinda akichaguliwa  kuwa Makamu wa Raisi wa Tanganyika Law Society kwa  mwaka 2023-2024 kwa kupata kura 527 kati ya kura 825.



Kwa upande wa mwekahazina nafasi imechukuliwa na Wakili Christopher Alex  kwa kupata kura 807 Kati ya Kura 825  


Pia  wakili Edward Heche  amechaguliwa kwa kuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Mawakili Vijana(AYL) wa TLS kwa  mwaka 2023-2024


Prof Hoseah atakabidhi kijiti rasmi baada ya kuitumikia TLS Kuanzia mwaka 2021 pia aliwahi kuwa Mkurugenzi wa Taasisi ya kuzuia na kupambana Rushwa (TAKUKURU) nchini Tanzania.

Chapisha Maoni

0 Maoni