Mbowe, Zitto, Marekani wamlilia Benard Membe


Baada ya salamu za pole kutoka kwa Rais wa Tanzania Samia kufuatia kifo cha Benard Membe Freeman Mbowe na Zitto Kabwe waeleza ya moyoni.

Rais Samia kupitia mtandao wa twita aliandika “ Nimepokea kwa masikitiko taarifa za kifo cha Ndugu Bernard Membe. Kwa zaidi ya miaka 40, Ndugu Membe alikuwa mtumishi mahiri wa umma, mwanadiplomasia, Mbunge na Waziri aliyeitumikia nchi yetu kwa weledi. Pole kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki. Mungu amweke mahali pema. Amina.”


Kwa upande wake Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe naye alimuelezea Membe na Nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya kifo cha aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje Mheshimiwa Bernard Membe. 



Zitto Kabwe ni kiongozi wa ACT Wazalendo ambapo kupitia chama hicho Benard Membe aliwania Urais mwaka 2020, ameandika Hakuna maneno yanayoweza kueleza mstuko mkubwa nilioupata kufuatia Taarifa ya msiba huu, zaidi ya kumshukuru Mungu muumba kwa Maisha ya Mzee wetu Bernard Kamilius Membe ambaye amefariki Dunia Leo asubuhi. 



Zitto amemtaja Membe kama Mwanasiasa mahiri, mwanadiplomasia maarufu na mwakilishi wa Wananchi. 

“Kwa niaba yangu Binafsi na kwa niaba ya Wanachama wa Chama cha ACT Wazalendo ambaye BM aliwahi kuwa mwanachama wake natoa pole kwa familia, ndugu, Jamaa, marafiki na Wananchi wote wa Jimbo la Mtama” ameandika 


Bolozi wa Marekani Tanzania Michael Battle naye ametuma salamu za pole 



Hamis Kigwangalla ameandika Siku zetu za kuishi hapa duniani ni chache sana. Wengi wanakutambua kama mwanadiplomasia, mwanasiasa nguli, kachero mbobezi, na mimi nakutambua kama mwanamikakati mwenzangu, propagandist na kaka/mentor wangu mkubwa kwenye siasa.

Chapisha Maoni

0 Maoni