Mstaafu Kikwete atema nyongo kuhusu Benard Membe

 

Rais mstaafu awamu ya nne Jakaya Mrisho Kikwete ametoa ya moyoni namna alivyomfahamu marehemu Benard Membe enzi za uhai wake .


Mstaafu Kikwete akitoa salamu zake wakati wa misa ya Kumuaga Marehemu Membe huko Lindi amesema Membe alikuwa jasiri na hakuogopa jambo lolote pale anapoona haliendi sawa hakusita kuonesha hisia zake.


Kikwete amesimulia wakati mgumu ambao alikutana nao katika urafiki wake na Membe ni kipindi alipoamua kuhama CCM na kuhamia ACT Wazalendo na baadae kuwania urais kupitia chama hicho.


Amesema ingawa ulikuwa ni uamuzi wake bila kushinikizwa  ulimpa wakati mgumu.


Ukweli uamuzi ule wa Membe ulinipa wakati mgumu wa kushirikiana naye lakini nashukuru baadae tulikuwa vizuri maana hasira zake ziliisha," amesema.



Amesema hata hivyo anajua familia moja inaweza kuwa na wanachama wa Chadema, ACT-Wazalendo, CUF, CCM lakini bado wanaendelea kushirikiana hivyo uamuzi wa Membe aliuchukulia wa aina hiyo.


Kikwete amesema  mara kadhaa alifanya jitihada za kutatua changamoto zilizomfanya Membe aondoke CCM na uamizi wa kurejea CCM ni miongoni mwa mafanikio ya jitihada zake.

Benard Membe ambaye aliwahi kushika nyadhifa mbalimbali ikiwemo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa ni mwanadiplomasia aliyezaliwa Novemba 9, 1953 alifariki dunia Mei 12, 2023 katika hospitali ya Hubert Kairuki alipokuwa akipatiwa matibabu.


Marehemu ameacha mjane na watoto watatu.

Chapisha Maoni

2 Maoni

Bila jina alisema…
Pumzika kwa aman membe
Bila jina alisema…
yatasemwa mengi sana