Uchunguzi bado kifo cha tata mwanafunzi UDOM

KIFO MWANAFUNZI UDOM

Bado uchunguzi wa kifo tata cha mwanafunzi wa UDOM Nusura Abdala haujakamilika wananchi watakiwa kuwa na subira.


Kauli hiyo imetolewa n Jeshi la Polisi nchini kupitia msemaji wake SACP David Misime wakati akijibu swali la mwandishi wa Mwananchi jijini Dodoma na kusisitiza jeshi likikamilisha uchunguzi litatoa taarifa.


Mtakumbuka katika taarifa yangu nilisema tukikamilisha tutawapa taarifa lakini hatujakamilisha na nisingetaka kuzungumza lolote kwasababu naweza nikawawekea maneno wanaochunguza wakaja na taarifa siyo za kiuchunguzi, naomba tuvute nsubira,”alieleza Misime


Marehemu Nusura Abddala ambaye alikuwa ni mwanafunzi shahada ya kwanza ya Sanaa katika Elimu, UDOM inadaiwa lifariki dunia akipatiwa matibabu katika hospitali ya Faraja Mkoani Kilimanjaro na kisha kuzikwa mkoani Singida.


Tarehe 3/5/2023 uongozi wa chuo ulipokea taarifa kutoka kwa mwanafunzi ambaye alikuwa anasoma naye kuwa amepokea taarifa kutoka kwa mtu aliyejitambulisha kuwa ni mjomba wa marehemu kuwa amefariki akiwa anapatiwa matibabu katika hospitali ya Faraja iliyopo Himo Kilimanjaro.


Chapisha Maoni

0 Maoni