Waziri Mkuu Majaliwa aongoza maziko ya Membe Lindi


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka wananchi kuenzi mazuri aliyofanya marehemu Benard Membe enzi za uhai wake.

Wito wa Waziri Mkuu Majaliwa ameutoa Mei 16, 2023 wakati akimuwakilisha  Rais  Samia Suluhu Hassan katika ibada ya mazishi ya marehemu Bernard Membe iliyofanyika kijijini kwake Rondo, Chiponda, mkoani Lindi.



Mwili wa Membe umezikwa katika makaburi ya Kanisa Katoliki Kata ya Chiponda, wakihudhuria viongozi mbalimbali akiwemo Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete, Waziri wa Tamisemi Angelah Kairuki na viongozi wengine.


Benard Membe ambaye aliwahi kushika nyadhifa mbalimbali ikiwemo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa ni mwanadiplomasia aliyezaliwa Novemba 9, 1953 alifariki dunia Mei 12, 2023 katika hospitali ya Hubert Kairuki alipokuwa akipatiwa matibabu.


Chapisha Maoni

0 Maoni