Kocha Nabi akiri ndani ‘ntiti’ nje ‘ntiti’ mechi Yanga Vs Marumo

 

Kocha mkuu wa Yanga  Nasreddine Nabi amesema timu yake imejiandaa kucheza nusu fainali dakika 180.

Amesema Marumo ni timu nzuri na kuwa wamejiandaa  kucheza na timu iliyofika hatua ya nusu fainali na sio nafasi yao kwenye msimamo wa ligi yakwao.


Akizungumzia maandalizi ya mechi yake dhidi ya Marumo Gallants ya Afrika Kusini kocha Nabi amesema “Hii ni mechi inayohitaji akili na tahadhari kubwa sana tunacheza mechi ya nyumbani lakini hauwezi kufuzu mchezo mmoja ni lazima tucheze tukiwaza dakika 180 za nusu fainali”


Hakusita kuwashukuru mashabiki wa timu hoyo na kusema “Niwashukuru sana mashabiki wa Yanga kwa sapoti mliyotupa kutoka mwanzo mpaka leo, nawaomba kesho tuongeze kitu kimoja”

“Kesho tushangilie kwa dakika zote 90, hata katika nyakati timu haina mpira tusiwe kimya, tupambane kushangilia ili kuwapa nguvu wachezaji wetu. Hii mechi sio nyepesi kama wengi wanavyodhani" amesema Nabi



Kwa upande wake golikipa  Metacha Mnata kuelekea mchezo huo amesema kila mchezaji anajua umuhimu wa mechi ya kesho, tunahitaji kuwa sehemu ya historia kubwa ya klabu “Tunaomba sapoti yenu mashabiki tukashinde pamoja”


Yanga inaratajia kushuka dimbani hapo kesho dhidi ya Marumo Gallants ya Afrikakusini ikiwa ni kusaka hatua ya kutinga fainali ya Kombe la shirikisho barani Afrika (CAFCC).

Chapisha Maoni

2 Maoni

Bila jina alisema…
Go yanga go yanga make the country proud
Bila jina alisema…
huo ntiti chacha utakuwa ni motooo