Tundu Lissu ashtushwa matundu 30 kwenye gari yake atoa maagizo




Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu amelitaka Jeshi la Polisi kuwatafuta waliofanya tukio la mashambulizi dhidi yake washughulikiwe kwa mujibu wa sheria.


Lissu ametoa wito huo akiwa katika Kituo kikuu cha Polisi Dodoma alipofika kwa mara ya kwanza kushuhudia  gari lake aliloshambuliwa nalo Septemba 7, 2017 na watu wasiojulikana.


Amesema  baada ya kufika kituoni hapo polisi walimpa fursa ya kuliona gari lake alilokuwa akilitumia siku aliyoshambuliwa na kujeruhiwa likiwa na matundu 30 ya risasi aliyoyahesabu.



“Yani nimehesabu yale matundu ya risasi nimeyaona 30, hii ni hatari sana, Hii gari imekuwa chini ya Polisi kwa muda wote huu na mimi binafsi nilikuwa sijawahi kuliona kabisa, nilikuwa nasikia tu kwamba nilipigwa risasi nyingi, leo wameniwezesha nimeona nashukuru kwa kulilinda gari hii,” amesema.



Septemba 7,2017 Lissu akiwa Mbunge wa Singida Mashariki, alifanyiwa shambulizi la risasi na wa watu wasiojulikana majira ya  mchana akiwa ndani ya gari, nje ya nyumba yake katika eneo la Area D, Site 3 mjini Dodoma.


Picha za gari hilo aina ya Toyota Land Cruiser VX, zilizopigwa baada ya tukio hilo, zinaonyesha likiwa na matundu zaidi ya 25 ya risasi; kwenye tairi la mbele upande wa abiria, na sehemu mbalimbali za upande huo ambao ndiyo aliokuwa amekaa mbunge huyo.

Matibabu 

Lissu baada ya shambulizi aliwahishwa katika hospitali ya rufaa ya Dodoma na baadae Nairobi na kuhamishiwa Ubeligi ambapo alipatiwa matibabu hadi afya yake kutengamaa.



Akiwa Nairobi Makamu wa rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ambaye kwa sasa ndiye Rais wa awamu ya sita alimtembelea kiongozi huyo alipokuwa akitibiwa.


Huku aliyekuwa rais wa awamu ya tano hayati John Magufuli akionesha masikitiko yake na kuvitaka vyombo vya dola viwasake wale wote waliohusika na tukio hilo la kinyama.

Chanzo:mwananchi/bbc/pichamtandao

Chapisha Maoni

3 Maoni

Bila jina alisema…
itabid aliuze tu apate jingine
Bila jina alisema…
Mzee mtata karudi tena
Bila jina alisema…
Huyu mwandishi ni kiboko hadi tweet ya magu kaidaka dah