Fataki, baruti marufuku uwanjani mechi ya Yanga Vs Marumo

 

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limepiga marufuku uwashaji na upigaji wa fataki uwanjani katika mechi kati ya Yanga na Marumo Gallants.

Kamanda wa Polisi Kanda maalumu ya Dar es salaam SACP Jumanne Muliro ametoa tahadhari hiyo na kusema jeshi linachukua tahadhari zote za kiusalama kabla, wakati na baada ya mchezo huo. 

“Jeshi la Polisi  linawatahadharisha baadhi ya mashabiki wenye tabia ya kuwasha fataki na baruti uwanjani, kurusha chupa au kitu chochote,hayo  ni baadhi ya makosa ya mambo ya kiusalama kwenye viwanja vya soka” amesisitiza SACP Muliro 


Akizungumzia Kamanda Muliro ameaema Usalama siku ya mchezo utakuwa wa kiwango cha juu maeneo yote ya kuzunguka uwanja ndani, nje na barabarani. 


“Hairuhisiwa mtu yeyote kwenda uwanjani na silaha ya aina yoyote , isipokuwa baadhi ya vyombo vya dola vyenye jukumu la usalama eneo hilo”

Chapisha Maoni

0 Maoni