Mwanamke amuua mumewe na kutunga kitabu cha kuwaliwaza wanawe

 


Mwanamke mmoja katika jimbo la Utah nchini Marekani ambaye amechapisha kitabu cha watoto kuhusiana na machungu ya kifo cha ghafla cha mumewe amefunguliwa mashtaka ya mauaji.

Mwanamke huyo Kouri Richins, mama wa watoto watatu, aliwaita polisi usiku wa manane Machi 2022 na kusema mumewe Eric Richins mwili wake ni wa baridi.

Mwanamke huyo alizieleza mamlaka kwamba alimuandalia mumewe mchanganyiko wa kinywaji aina ya vodka, na kumkuta hana uhai saa nne baadae.

Uchunguzi wa kitabibu baadae uling’amua kwamba marehemu Eric kifo chake kilisababishwa na kuzidisha dozi ya dawa kali ya maumivu aina ya fentanyl.

Bi. Kouri alipata dawa za fentanyl na kisha kuwa anamchanganyia mumewe kwa lengo la kumuua, ambapo rafiki mmoja wa Eric alidai marehemu alimueleza anahisi mkewe anamuwekea sumu.

Chapisha Maoni

0 Maoni