Makaburi ya waumini waliokufa wakutane na Yesu yazidi kubainika

 


Waziri wa Mambo ya Ndani wa Kenya Prof. Kithure Kindiki ameelezea vifo vya waumini wa dhehebu la dini ya Kikristo eneo la Shakahola kuwa ni uhalifu uliopangiliwa.

Waziri huyo ametoa kauli hiyo leo alipowasili Malindi mkoa wa Pwani kusimamia zoezi la kufukua makaburi, ambalo lilisitishwa wiki iliyopita kutokana na hali mbaya ya hewa.

“Ninahofia kwamba tuna makaburi mengi,” Prof. Kindiki alisema na kuongeza kwamba ufukuaji wa makaburi unaweza kuchukua muda mrefu kuliko ilivyotarajiwa.

“Uharibifu uliofanywa upo dhahiri, makaburi 20 walimozikwa watu wengi kwa sasa yamefukuliwa. Mchakato wa kufukua makaburi sio wa kuisha hivi karibuni,” alisema Prof. Kindiki.

Hadi sasa miili ya watu 112 hadi sasa imepatikana na vifo vyao vimethibitishwa, huku Mchungaji wao Paul Mackenzie, na mchungaji mwingine Ezekiel Odero wakiendelea kushikiliwa na polisi.

Chapisha Maoni

0 Maoni