Dk Dugange hajajiuzulu taarifa yatoa onyo


Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) imekanusha taarifa inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii ikimuhusisha Naibu Waziri Ofisi ya Rais - TAMISEMI anayeshughulikia Afya, Dkt. Festo Dugange kuwa amejiuzulu wadhifa wake ili kupisha uchunguzi.


Taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano- TAMISEMI, Nteghenjwa Hosseah imesema kwamba taarifa zinazoeleza kuwa Naibu Waziri amejiuzulu ni uzushi na Wananchi wanaombwa kuipuuza kwani Dkt. Dugange hajajiuzulu wadhifa wake huo bado ni Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI na Mbunge wa Jimbo la Wang'ingombe Mkoani Njombe.

“Kwa sasa anaendelea kupatiwa matibabu kwenye Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Benjamini Mkapa iliyoko Jijini Dodoma kufuatia ajali ya gari aliyoipata usiku wa tarehe April 26,2023” ilibainisha taarifa hiyo 

ACT Wazalendo 

Awali iliyolewa taarifa ya chama cha ACT Wazalendo ikihusisha Utata kifo cha Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM); na minong’ono ya mtandaoni kubusu Naibu Waziri Dk Dugange  na kumtaka ajiuzulu ili kupisha uchunguzi.

Polisi waonya

Msemaji wa Jeshi la Polisi Tanzania SACP David Misime katika taarifa alisema jeshi hilo limebaini kuwepo kwa taarifa katika mitandao ya kijamii ikihusisha kifo hicho na ajali ya gari iliyotokea jijini Dodoma ikimuhusisha Naibu waziri Tamisemi Dk Festo Dugange.

TAZAMA VIDEO

Katika taarifa SACP Misime ilisema  jeshi la polisi mkoani Kilimanjaro baada ya kuwepo kwa taarifa hizo imeanza kufanya uchunguzi kwa watu mbalimbali ikiwemo hospitalini alipotibiwa binti huyo na kushirikisha ofisi ya mkemia mkuu, DPP na wadau wengine wa haki jinai.

Chapisha Maoni

2 Maoni

Bila jina alisema…
Jamani hili sakata linafunikwa sana kwakweli mama aamue tu kumpumzisha ataupiga mwingi
Bila jina alisema…
Sio vyema kulinda mauzinzi jaman kama nj kwelikama ni wongo yaishe