Waziri Tax aeleza safari ngumu ya kuwaokoa Watanzania Sudan hadi kurejea Tanzania


Watanzania 206 wamewasili nchini katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) kutokea Sudan huku Serikali ikisema bado inaendelea na jitihada za kuwatafuta wengine waliobakia kuwarudisha nchini.

Akizungumza Dar es Salaam na vyombo vya habari leo Alhamisi,  Aprili 27,2023 katika hafla ya mapokezi hayo, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk Stergomena Tax amesema kazi kubwa imefanyika hadi kuwapata Watanzania hao.



Kutokana na changamoto hizo Dk Stergomena amewataka  Watanzania wote wanaoishi mataifa ya nje kujisajili kwenye ubalozi ili iwe rahisi kuwasaidia.


Mpaka sasa ni Watanzania wanne pekee  wamebaki nchini Sudan huku jitihada zikiendelea kufanyika kuwanusuru.



Waziri Tax ameeleza kuwa  safari ya kurejea nchini ya Watanzania hao, ilianza tarehe 24 Aprili 2023 kutoka Jiji la Khartoum, Sudan hadi mpaka wa kimataifa wa Metema uliopo kati ya Sudan na Ethiopia ambao ni umbali wa takribani kilomita 900. 


Baada ya hapo, tarehe 26 Aprili 2023, Ubalozi wa Tanzania nchini Ethiopia uliratibu usafiri kutoka mpaka wa Metema hadi mji wa Gondar takriban kilomita 190. Kutoka Gondar, ujumbe huo ulisafiri kwa ndege ya Shirika la Ndege la Ethiopia kuelekea Addis Ababa. 



Ndege mbili zilitumika ambapo ya kwanza ilisafirisha watu 135 na ndege ya pili ilisafirisha watu 95.  Kutoka Jijini Addis Ababa, wananchi hao walisafiri kwa ndege ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) hadi Jijini Dar es Salaam.

Chapisha Maoni

0 Maoni