Rais Samia Suluhu Hassan amesema mazungumzo yake na Rais Paul Kagame wa Rwanda yamejikita katika mambo mbalimbali ikiwemo biashara, Mawasiliano na Ulinzi na Usalama.
Akizungumzia kuhusu biashara Rais Samia amesema “Tumeona haja ya kukuza biashara na kuweka miundimbinu ya kukuza biashara kwasababu kiwango cha biashara tulichonacho hakiendani na rasilimali tulizonazo kwa nchi mbili lakini na uhusiano uliopo”
Kwenye upande wa Mawasiliano amesema “Tumeangalia jinsi ya kuimarisha njia nyingine za mawasiliano ili Tanzania iweze kutoa huduma kwa ufanisi kule Rwanda na nchi nyingine zinazotuzunguka”
“Tumezungumzia pia suala la mradi wetu wa Rusumo ambao tumeshukuru unaendelea vizuri na tumekubaliana tunakwenda kuuzindua kwa pamoja”.
0 Maoni