Chanzo cha kifo cha bondia aliyedondoka ulingoni chatajwa


Mwili wa bondia  wa ngumi za kulipwa nchini Ibrahim Najum Mwakalebela umesafirishwa Mkoani Mbeya kwa ajili ya maziko.

Mwakalebela  alifariki dunia mchana wa April 27  katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Dodoma alipokuwa akipatiwa matibabu baada ya kuanguka  ulingoni katika tamasha mkoani Dodoma  baada tu ya kumaliza  raundi nne dhidi ya bondia wa Dodoma Laurent Segu maarufu kwa jina chatu.

Akithibitisha kifo cha bondia huyo mwandaji wa tamasha la uchangiaji wa pedi za kike na Mbunge wa viti Maalumu Sophia Mwakagenda alisema kuwa awali bondia huyo alipoanguka aliwahishwa hospitali kwaajili ya matibabu.

Siku ya pili walitaatofiwa kuwa daku haijaingia kwenye ubongo na angefanyiwa upasuaji na alifanyiwa na hali yake iliendelea vizuri chini ya uangalizi lakini jana mchana alifariki dunia.

Kihistoria bondia  huyo alikuwa amecheza mapambano matatu ya ngumi za kulipwa ambapo ameshinda Moja na kupoteza mawili.

Chapisha Maoni

0 Maoni