Uhaba wa mafuta wafuta sherere za Mei Mosi Cuba

 


Serikali ya Kikomonisti ya Cuba imefuta maandamano ya sherehe za Siku ya Wafanyakazi Duniani, Mei Mosi kutokana na uhaba mkubwa wa mafuta.

Kila mwaka mamia kwa maelfu ya watu hufurika katika kila kona ya kisiwa hicho na kujaza eneo la mapinduzi la Havana Square katika kuadhimisha Siku ya Wafanyakazi Duniani.

Kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1959 ya mapinduzi ya Cuba, sherehe hizo za Mei Mosi zimefutwa kwa sababu za kiuchumi.

Katika siku za hivi karibuni kumekuwa na foleni ndefu kwenye vituo vya mafuta, ambapo madereva wamekuwa wakingojea kupata bidhaa ya mafuta kwa siku kadhaa.

Mapema mwezi huu, Rais Miguel Diaz-Canel amesema Cuba imekuwa ikipata theluthi mbili tu ya mafuta inayoyahitaji, na kuongeza kuwa wasambazi wamekuwa hawatimizi matakwa ya mikataba yao.

Chapisha Maoni

0 Maoni