Katika Droo ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho barani Africa (CAFCC) Yanga SC atakipiga na Marumo Gallants ya Afrika ya kusini.
Mchezo wa kwanza katika hatua ya nusu fainali Yanga wataanzia nyumbani Benjamin Mkapa mnamo Mei 10, 2023 na mchezo wa marudiano utakuwa ni huko Afrika Kusini Mei 17, 2023.
Wengine watakaokiputa kuingia fainali ni Asec Mimosas ya Ivory Coast wakikipiga na USM Alger.
Klabu ya Yanga ilitinga hatua ya nusu fainali kufuatia ushindi wa jumla wa 2-0 dhidi ya miamba ya Nigeria, Rivers United.
Huku Marumo Gallants ya Afrika Kusini ikitinga kwa kuwachabanga miamba ya Misri Pyramids kwa ushindi wa jumla wa 2-1.


0 Maoni