Watu wahaha bandarini kukimbia machafuko Sudan

 


Bandari ya Sudan imekuwa ni eneo muhimu kwa maelfu ya watu wanaokimbia machafuko ya Sudan.

Maafisa wa Saudi wamekuwa wakihaha kutafuta njia salama ya kuowaondosha watu wanaokimbia Sudan kupitia bandari hiyo.

Majira ya saa mbili asubuhi vyombo viwili vya majini viliruhusiwa kuondoka bandari ya Sudan ambayo ni bandari kubwa ya nchi hiyo.

Wengi wanaokimbia machafuko wanahofia kutoweza kutoka nchi hiyo.

Bandari ya Sudan imefurika watu wasio na hati za kusafiria wengi wao wakitoka nchi za Yemeni, Syria na Wasudani wenyewe.

Baadhi ya raia wa Yemen 3,000 wengi wao wakiwa ni wanafunzi wamekwama kwenye bandari ya Sudan.



Chapisha Maoni

0 Maoni