Manchester City yakwea kileleni ligi ya EPL

 


Manchester City imeifunga Fulham na kukaa kileleni mwa Ligi Kuu ya England wakati Erling Haaland akifunga goli lake la 50 la msimu huu katika michuano yote.

Haaland alifunga goli hilo kwa mkwaju wa penati katika dakika ya tatu, baada ya Julian Alvarez kufanyiwa madhambi na Tim Ream. City waliibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya Fulham.


Bruno Fernandes amefunga goli lake la 100 na kuimarisha matumaini ya Manchester United kushiriki ligi ya mabingwa Ulaya kwa kuifunga Aston Villa goli moja kwa bila.

Frenandes alifunga goli dakika sita kabla ya mapumziko, baada ya Emiliano Martinez kuzuia shuti la Marcus Rashford.



Goli la Diogo Jota lililofungwa dakika za majeruhi limeipatia ushindi timu ya Liverpool wa magoli 4-3 dhidi ya Tottenham.

Chapisha Maoni

0 Maoni