Rais wa Rwanda Paul Kagame ahitimisha ziara yake ya Kikazi nchini

 

Rais wa Rwanda Paul Kagame amehitimisha ziara yake ya kikazi ya siku mbili nchini Tanzania nakurejea nchini Rwanda Leo


Mhe. Kagame ameagwa katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam na Waziri wa Mambo ya Nje Dkt Stergomena Tax ambaye aliambatana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais IKULU-Zanzibar Mhe Jamal Kassim Ali na Waziri wa Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe,Nape Nnauye 



Viongozi wengine waandamizi wa Serikali waliomsindikiza ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Amos Makala,Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje Balozi Samwel Shelukindo,Balozi wa Rwanda nchini Tanzania Meja Jenerali Charles Karamba pamoja na Mkurugenzi wa idara ya Afrika kutoka Wizara ya Mambo ya Nje Balozi Naimi Aziz

Chapisha Maoni

0 Maoni