Wydad yaichapa Simba kwa mikwaju ya penati 4-3

 

Mabingwa watetezi wa ligi ya mabingwa Afrika Wydad Casablanca wameiondoa Simba katika mashindano ya ligi ya mabingwa kwa mikwaju ya penati 4 kwa 3.

Mechi  Ligi ya Mabingwa kati ya Simba SC dhidi ya Wydad  Casablanca ilipigwa majira  saa 4:00 usiku kwa saa za Tanzania, ambapo ilikuwa saa 2:00 kwa saa za Morocco, katika uwanja wa Mohamed V mji wa Casablanca.



Baada ya dk 90 ikiwa ni 1-1 baada ya goli la Simba la nyumbani na kunyukwa moja na Wydad ikafuatiwa mikwaju ya penati ambapo simba kupitia wachezaji wake Shomari kapombe na Clatous Chama walikosa penati na kuipa Wydad ushindi wa 4 kwa 3.


Mchezo huo ulikuwa ni nafasi ya kipekee kwa Simba kutinga nusu  fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kuingia mguu mmoja katika ushindi wake nyumbani dhidi ya mabingwa watetezi Wydad.


Katika kuongeza hamasa Rais Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan ameongeza motisha kwa timu za Simba na Yanga kutoka shilingi milioni 5 hadi shilingi milioni 10 kwa kila goli litakalofungwa na timu hizo endapo zitafanikiwa kufuzu kucheza Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa (Simba) na Kombe la Shirikisho (Yanga).


Timu iliyobaki ni Yanga katika kombe la shirikisho ikisubiriwa kwa hamu kama itaweza kupeperusha bendera ya taifa katika anga za kimataifa.


Chapisha Maoni

0 Maoni