Ujenzi wa daraja la Dar -Zanzibar lazua gumzo bungeni,serikali yafafanua

Serikali imeanza mazungumzo na Kampuni ya China Overseas Engineering Group Company (COVEC) ambayo imeonesha nia ya kuwekeza katika ujenzi wa daraja litakalo unganisha Tanzania Bara na Zanzibar.

TAZAMA VIDEO

Naibu Waziri wa Uchukuzi Godfrey Kasekenya amesema bungeni leo Aprili 28, 2023 kuwa Mazungumzo hayo yameanza Machi 11, 2023 na yalihusisha wataalamu kutoka Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi Sekta ya Ujenzi kwa upande wa Tanzania Bara na Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi kwa upande wa Zanzibar.


Akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Mwantum Dau Haji  aliyetaka kujua mpango wa serikali kujenga daraja hilo, Naibu Waziri Kasekenya amesema bado mazungumzo yanaendelea na serikali inakusudia kujiridhisha na teknolojia zinazotumika katika ujenzi wa madaraja makubwa kabla ya kuanza ujenzi.


“Daraja hili litajengwa kwa kushirikiana na sekta binafsi kwa utaratibu wa PPP (Public-Private Partnership),” amesisitiza Kasekenya.

Chapisha Maoni

0 Maoni