Makombora ya Urusi yaua watu 13 Ukraine


Urusi imeanzisha mashambulizi ya mfululizo ya makombora kwenye miji ya Ukraine, ukiwamo mji wa Kyiv na kusababisha vifo vya watu wapatao 13.

Maafisa wa Ukraine wamesema watu 11 wakiwamo watoto wameuawa katika shambulizi la makombora yaliyolenga ghorofa katika mji wa kati wa Uman.

Pia, mwanamke mmoja pamoja na binti yake wa miaka mitatu waliuawa katika mji wa Dnipro, kwa mujibu wa meya wa mji huo.

Milipuko mingine pia imeripotiwa kusikika katika mji wa Kremenchuk kati kati ya Ukraine.

Chapisha Maoni

0 Maoni