Mashimo ya barabara za Kampala ya-trend

 

Mashimo makubwa yaliyopo kwenye barabara nyingi za Uganda katika jiji la Kampala yamegonga vichwa vya habari kwa watu kuyaposti kwenye mtandao wa twitter kiasi cha ku-trend.

Wakitumia #KampalaPotholeExhibition, wakazi wa jiji hilo wamekuwa wakitupia picha za mashimo ya barabarani ambayo magari yao inabidi kukabiliana nayo ili kupita barabarani.

Baadhi ya mashimo hayo ya barabarani yalionekana kama ni ramani za kijiographia, yakiwa na muonekeano wa mito midogo kila inyeshapo mvua.

Mamlaka ya Jiji la Kampala KCCA imekiri kuwapo kwa tatizo hilo, ambalo linaukubwa wa eneo la mita za mraba 8,500.

KCCA imesema kwamba barabara hizo zimefikia muda wa kufanyiwa ukarabati, na ndio maana kuna uwapo wa mashimo hayo na uharibifu mwingine.

Magari yakijaribu kuyakwepa mashimo makubwa yayojaa maji katika moja ya barabara zilizoharibika katika jiji la Kampala.

CHANZO: BBC

Chapisha Maoni

0 Maoni