Chelsea si riziki tena mwaka huu

 

Matumaini ya Chelsea ya kufanya vyema msimu huu yamezimwa kikatili na Real Madrid, kwa kipigo cha magoli 2-0 katika dimba la Stamford Bridge na kutolewa kwa jumla ya magoli 4-0, na Real Madrid kusonga mbele katika hatua ya nusu fainali ya ligi ya mabingwa Ulaya.

Chelsea ambao walikuwa wakihaha kubadili matokeo ya magoli 2-0 waliyofungwa katika mchezo wa awali uliopigwa katika dimba la Bernabeu, walijikuta wakishindwa kufanya vyema huku wakishindwa kutumia nafasi za kufunga za wazi.

Kiungo N'Golo Kante alikosa nafasi ya kufunga katika kipindi cha kwanza, huku mpira wa Marc Cucurella ukizuiliwa na kipa wa zamani wa Chelsea Thibaut Courtois wakati amapo ilionekana kama angeweza kuwachanganya Real.

Nayo timu ya AC Milan ya Italia imefanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo kwa mara ya kwanza baada ya kupita miaka 16, kwa kuibuka na ushindi wa jumla ya mabao 2-1 dhidi ya Napoli.

CHANZO: BBC

Chapisha Maoni

0 Maoni