Mzee aliyempiga risasi kijana mweusi ajisalimisha

Mzee wa miaka 84 mkazi wa jimbo la Missouri nchini Marekani, amejisalimisha polisi baada ya kumpiga risasi kijana mweusi aliyegonga kimakosa kengele ya mlango wa nyumba yake.

Mzee huyo Andrew Lester aliachiwa kwa dhamana baada ya kushtakiwa kwa makosa ya kukusudia kuua kwa kutumia silaha na kutumia silaha kufanya uhalifu.

Mzee huyo mzungu alidaiwa kumpiga risasi Ralph Yarl, 16, kijana mweusi, moja kichwani na nyingine mkononi katika mji wa Kansas.

Hata hivyo kijana huyo Ralph Yarl hakufa na madaktari wamesema kwamba hawajui ni kwa vipi amenusurika kifo.

CHANZO: BBC

Chapisha Maoni

0 Maoni