Wanafunzi 171 Wakwama Sudan, Serikali Yatoa Tamko Kusitishwa Vita

 


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt Stergomena Tax amesema zaidi ya raia wa Tanzania 210 wamekwama nchini Sudan kufuatia vita inayoendelea.


Waziri Tax ameyasema hayo Leo Aprili 19 bungeni wakati akitoa tamko la serikali kuhusu vita inayoendelea nchini humo.

“Serikali imeendelea kufanya mawasiliano mara kwa mara na ubalozi wetu ili kujua hali inavyoendelea 171 kati ya hao ni wanafunzi ,wengine ni maafisa wa ubalozi na raia wengine” alisema 


TAMKO LA SERIKALI 

Katika tamko la nchi kupinga mapigano hayo Waziri Tax amesema Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inasikitishwa na hali ya kuzorota kwa amani na usalama inayoendelea.


Tanzania ikiwa kama mjumbe wa baraza la amani na usalama la Umoja wa Afrika inaunga mkono tamko lililotolewa na baraza hilo katika kulaani mapigano hayo na kutoa wito kwa pande zote mbili kusitisha mapigano hayo.

TAZAMA VIDEO

Waziri Tax alisema Tanzania inazitaka pande zote mbili zinazohasimiana kutatua mgogoro kwa njia za amani na usalama huku zikihakikisha mahitaji ya kibinadamu kwa raia na raia wa kigeni. 

VITA ILIPOANZA

Tarehe 15 mwezi April  nchini Sudan kulizuka mapigano kati ya vikosi vya serikali na vikosi vya msaada katika mji mkuu wa Sudan Khartum na katika maeneo mbalimbali nchini humo.


Mapigano hayo yamesababisha vifo 185, majeruhi zaidi ya 1,000 na uharibifu wa mali ikiwemo ndege.


Mapigano hayo yanatajwa kuchangia kurudisha nyuma  huku jitihada mbalimbali zikiendelea katika kutafuta suluhisho baina ya wapiganaji hao.

Chapisha Maoni

0 Maoni