Mapigano ya kuwania madaraka yaua watu 50 Sudan

Mapigano ya kuwania madaraka baina ya jeshi la Sudan na kikosi cha jeshi korofi yameitingisha nchi hiyo na kusababisha vifo vya raia 50.

Wakazi wa Jiji la Khartoum wamejikuta wakikwepa risasi, wakati majeshi hayo yakipigana kutwaa ikulu, televisheni ya taifa pamoja na makao makuu ya jeshi.

Watu 25, wakiwamo raia 17 wamekufa katika Jiji la Khartoum, shirikisho moja la madaktari nchini humo limesema.

Mapigano hayo yameibuka kufuatia kuwapo kwa mapendekezo ya kipindi cha mpito kuelekea utawala wa kiraia.

Jeshi la Sudan pamoja na jeshi kinzani la Rapid Support Forces (RSF), wote wamedai kushikilia miji muhimu, ambayo mapigano yanaendelea.

Silaha nzito zimesikika mji wa Omdurman, uliokaribiana na Khartoum, na karibu na Bahri jumapili majira ya asubuhi. Mashahidi wameripoti kutokea milio ya risasi mji wa Red Sea wa Port Sudan.

Ndege za jeshi zimeshambulia kambi za RSF, ambapo vikosi vya anga vya nchi hiyo viliwaagiza watu kukaa majumbani mwao usiku wa jumamosi wakati vikiendesha operesheni ya anga.

Watu wapatao 56 wamekufa katika miji kadhaa na mikoa nchini humo, huku kamati ya madkatari wa Sudan ikisema makumi ya wanajeshi wamekufa. Watu 595 wamekufa.

Chanzo: BBC

Chapisha Maoni

0 Maoni