Mwanasiasa India apigwa risasi live akiongea kwenye TV

 
Mwanasiasa wa nchini India aliyetiwa hatiani kwa utekaji nyara amepigwa risasi na kufa wakati akiongea mubashara kwenye runinga pamoja na ndugu yake wa kiume.

Atiq Ahmed, ambaye alikuwa akisindikizwa na polisi, alikuwa akiongea na waandishi wa habari wakati mtu mmoja alipotoa silaha na kumfyatulia risasi kichwani huko Prayagraj.

Baada ya kufyatua risasi hiyo mwanaume mmoja aliyejichanganya na waandishi wa habari alijisalimisha mara moja na anashikiliwa na polisi.

Mtoto wa kiume wa mwanasiasa huyo Ahmed aliuawa kwa kupigwa risasi na polisi siku chache zilizopita.

Siku za nyuma mwanasiasa huyo mhalifu Ahmed alidai kuwa kumekuwapo na tishio la kuuawa na polisi.

Video iliwaonyesha Ahemd na kaka yake Ashraf, wakiwa wamefungwa pingu, wakiongea na waandishi wa habari wakielekea kupimwa afya hospitali sekunde chache kabla ya kuuawa.

Chanzo: BBC

Chapisha Maoni

0 Maoni